TEKNOLOJIA YATUPONZA

Imelemaza dunia,teknoloji yatuponza
Mitandao twatumia,ubongo inatufyonza
Hatuwezi fikiria,akili imepumbaza
Teknoloji yatuponza,dunia imelemaza.

Uzembe metuingiya,kazi zimetulemea
Njaa inatuvamiya,kublogi twaendelea
Biashara zafifiya,kukopa tumezoea
Teknoloji yatuponza,dunia imelemaza.

Masomo yanadorora,wasomi wamezembea
Kaziyo kuposti sura,insta wanapotelea
Wataja kuwa wakora,hivi wakiendelea
Teknoloji yatuponza,dunia imelemaza.

Kuta zimejenga simu, kwa watoto na wazazi
Mitandao instagramu,twita piya kitandazi
Muwiko hata salamu,mkondoni wako bizi
Teknoloji yatuponza,dunia imelemaza.

Simu ndizo tunaenzi,pili twapenda vipeni
Hayapo tena mapenzi,wapenzi hatupendani
Waponza utandawazi, hulka hasi kileteni
Teknoloji yatuponza,dunia imelemaza.

Share this

2 thoughts on “TEKNOLOJIA YATUPONZA

  1. Kazi nzuri rafiki.
    Jua liking’aa tutakuja kalia meza ya kifahari tukitabasamu huku tukiwa na taswira ya mapito na changamoto za maisha. Kwani upo wakati tutafanikiwa.
    Heko Gatumo

Leave a Reply

Your email address will not be published.