RAFIKI WANGU WA SIRI.

Meishi naye kwa muda, na bado upo usena.
Sikiza kaka na dada, nimeamua kunena.
Zaidi zingatia mada, penzi lake naliona.
Rafiki wangu wa siri, Mola aleniumba.

Atuita kila Mara, bado tusijafika kilele.
Hana nyingi papara, au zile kelele.
Tukimbie kama swara, uzimani wa milele.
Rafiki wangu wa siri, Mola aleniumba.

Ata bila hivyo vyeti, maishani utapata.
Neno lake ndo tikiti, latwepusha matata.
Cha enzi chake kiti, anang’aa ja nyota.
Rafiki wangu wa siri, Mola aleniumba.

Havutiwi majivuno, apendacho ni upole.
Tuhubirini hili neno, zawadi ziko mbele.
Ata kama huna meno, upo uzima milele.
Rafiki wangu wa siri, Mola aleniumba.

ALSO READ:  NDOTO YA AJABU.

Upigwapo navyo vita, silipize anasema.
Mapito tutayapita, ila daima twasimama.
Mibaraka tutapata, kwake nami nitazama.
Rafiki wangu wa siri, Mola aleniumba.

Anatuvusha matatizo, kila mara hutupenda.
Kwake hakuna likizo, tumwamini tutashinda.
Kwake lipo liwazo, ‘ta milima tukipanda.
Rafiki wangu wa siri, Mola aleniumba.

Mfanye leo rafiki, hutojutia daima.
Tumwambie tamalaki, atatupa na uzima.
Aongeza pia maki, pasiwe na lalama.
Rafiki wangu wa siri, Mola aleniumba.

Mikono yangu nanawa, keshafanya mahubiri.
Alipenda naye Hawa, yuaja tumsubiri.
Jina lake pia dawa, limeze utanawiri.
Rafiki wangu wa siri, Mola aleniumba.

Share this

Leave a Reply

Your email address will not be published.