LIPI LA KWELI? Kupona korona kwa Brenda na Brian kwaibua hisia mseto.


Maswali chungu nzima yaibuka miongoni mwa wakenya baada ya “mashujaa” wa korona kutoa habari kinzani.

Kulingana na uchunguzi wa hivi punde habari hizi zimeenea mithili ya moto wa nyika.

Wengi wao wamejitokeza hadharani kusuta ,kukejeli na kuonyesha kutoamini ukweli huu.

Mnamo jana tarehe 1/04/2020, vyombo vya habari vilipeperusha moja kwa moja ushuhuda waliotoa Ivy Brenda Cheroitich na mwenziwe Brian .

Wote kwa pamoja walionekana kujawa na furaha riboribo baada ya kupata shufaa na hatima kupona gonjwa hili la korona( Covid-19).

Rais wa taifa la Kenya Uhuru Kenyatta aliwasiliana nai moja kwa moja kutoka ikulu ya rais nao waathiriwa pamoja na waziri wa afya MUTAI KANGWE miongoni mwa matabibu wengine wakiwa katika jengo la AFYA HOUSE.

MASWALI YAWALAO WAKENYA NI; Je, kama kisa cha kwanza cha korona kuripotiwa humu nchini kilitanganzwa mnamo tarehe 13 /03/2020, idadi ya siku itafikiaje 23 kama walivyodai kuwa karantini?

Idadi ya siku kamili kutoka kisa cha kwanza adi jana 1/04/2020.

Ni siku 19 wala si 23.

Brenda ana miaka mingapi? Kulingana na ripoti ya Kangwe alipotangaza kisa cha kwanza , muathiriwa alikwa na umri wa miaka 27.

Hii ilikinzana na matamshi ya Brenda kwamba ana miaka 26.

Je, Brenda alipataje namba ya msafiri katika ndege?

Wengi wanakiri kwamba ni nadra kwa abiria kuitishana namba za simu ikizingatiwa kuwa hawafahamiani.

Brian ni nani kwa Brenda? Akihojiwa katika televisheni ya NTV Jana, Brenda alikiri kuwa alikuwa mpenziwe.

Alipohojiwa katika televisheni ya Citizen, Brenda aliapa kutomjua kijana huyu.

Kulingana na yeye, alimuona Mara nadra katika nyumba.

Brenda alitumiaje kipakatalishi hospitalini?

Katika maongezi yake jana, alidai kutumia chombo hiki, kitabu na kalamu kunukuu baadhi ya achowaza akiwa amelazwa.

Je, inawezekana mtu aliye lazwa kuwa na uhuru huu?

HAIDHURU; Kwa sasa twapasa kumtegemea Mungu, kuyafuata maagiza watoayo matabibu ikiwemo kutumia vyeuzi, kunawa mikono kutumia sabuni na maji kwa muda wa sekunde ishirini na kukaa nyumbani.

USHAIRI WANGU KWAKO.

Yaepuke mapuuza, Nawa mikono, kwepa salami za mkono abadan kataan , kula vyema na usisahau Biblia yako.

Share this

6 thoughts on “LIPI LA KWELI? Kupona korona kwa Brenda na Brian kwaibua hisia mseto.

 1. I like this brother,,,
  Products of Egerton University
  Through prayer and supplication God will expand your territories

 2. I’m truly enjoying the design and layout of your blog.
  It’s a very easy on the eyes which makes it much more pleasant for me to come here and visit more
  often. Did you hire out a designer to create your
  theme? Outstanding work!
  That is why I want to share with you what motivated me to
  develop and earn money, maybe it will help
  someone: https://bit.ly/2ULpwNj

  1. Am really numbed .
   I do all the work you see here and wish to do more . Am happy that a can touch a soul by passing messages in deferent styles.

Leave a Reply

Your email address will not be published.