NEWS SPORTS

DARUBINI LIGI KUU TANZANIA, MACHACHE YA AZAM FC

Klabu ya Azam Fc imemaliza msimu huu ikiwa kwenye nafasi ya 3 kwa mara nyingine na kuendelea kuzua maswali juu ya malengo klabu hiyo kwa misimu ya karibuni.

WALIKWAMA WAPII!?

Ettienne Ndayiragije. Azam ilianza msimu ikiwa chini ya Ndayiragije na alishatengeneza lengo lake la msimu kabla ya kutwaliwa na TFF akahudumu kwenye timu ya taifa. Azam FC ikahudumiwa na Mingange kwa muda Kisha akaja Cioaba.

Mabadiliko ya benchi la ufundi yaliiathiri Azam jumla kwani wachezaji wamelazimika kuziishi falsafa tatu kwa muda mfupi. Isingekua rahisi kwa Azam kutwaa ubingwa bila mwanzo mzuri.

Wachezaji. Wachezaji wao wengi hawakuwa kwenye ubora zoeleka. Timu ilikua ilikua na makosa binafsi mengi zaidi kwa wachezaji mmoja mmoja. Abalora, Yakub, Chilunda n.k ni mfano tu Ila wengi wao hawakuwa na mwendelezo wa ubora.

ALSO READ:  ERECT BANDA TO AVOID POSSIBLE CONTAMINATION OF FISH BY CORONA VIRUS COUNTY URGED.             

Wachezaji na ari ya upambanaji. Kwa sasa humuoni Kipre Tcheche, Eid Mwaipopo, Hamis Mcha, Vladimir Niyonkuru, Shikanda, Ndeule, Tumbo ama Bocco kwenye kikosi Chao… Wamekosa wachezaji viongozi na Ari ya wachezaji wao ina shaka kwa sasa.

Mechi za Ugenini zilikua ngumu zaidi kwao. Hawakuonesha ukubwa kwenye viwanja vigumu.

INASEMEKANA Azam inaishi kama mtoto wa kambo VPL. Sina hakika lakini Msimu huu ni wachezaji wenyewe.

WAPI WALIKUWA BORA!?

Idara ya Habari ya Azam FC imefanya vyema. Utoaji wao wa taarifa na uendeshaji wa mitandao ya kijamii unanivutia zaidi. Ndio timu yenye mpiga picha bora Tanzania kwa sasa.

Kimasoko wamefanikiwa Sana. Huu ndio msimu ambao Azam wameuza zaidi jezi kwenye mikoa mingi na kuweka mawakala wengi. Kongole kwa idara yao ya masoko. Klabu imeongeza mashabiki pia.

ALSO READ:  "Huyu William Ruto aanze kujipanga nje ya Jubilee." Brian Weke

Hata kumaliza 3 Bora ni Jambo la kheri ingawa tunaona si vyema kwa matarajio tuliyobeba kwa Azam.

NINI KIFANYIKE!?

Usajili. Scouting ya Azam kwa Sasa iwe makini kwa wachezaji wanaowasajili hususani wazawa kwani kwa siku za karibuni imesajili wakamiaji. “Tunasajili mchezaji lakini hafanyi vyema kumbe huenda alitukamia tu sisi” CEO Nurdin Popat. Wasajili kwa tija.

Warudi kwenye malengo Yao ya awali. Azam sio timu ya kupambania nafasi ya 2 au 3… Ni timu inayoshawishi kupambania ubingwa zaidi.
Wasalaam

Nazareth J Upete
Nazareth J Upete
Nazareth Upete is a young Tanzanian journalist who believes in collective development, transparency, fairness and dignity. He is specialized in Sports and News writing. An anchor, reporter, analyst and columnist.

Leave a Reply

Your email address will not be published.