SHAIRI LA WIKI.

WALEVI KUPIGWA KUMBO

Pigo nalo wamepata, wengine kunusurika.
Vitapungua vita , boma nyingi taimarika.
Habari nayo kapata, wamewekewa mipaka.
Tabasamu la wengi, walevi kupigwa kumbo.

Walifanya mzaha, kadhani wamefika.
Rais kwa madaha, kasema amechoka.
Sasa hawana raha, macho yamewatoka.
Tabasamu la wengi, walevi kupigwa kumbo

Walisumbua polisi, tukabaki tukimaka.
Wakadhani rahisi, serikali kawasaka.
Ndio huo wasiwasi, milango kufungika.
Tabasamu la wengi, walevi kupigwa kumbo

Mitaroni walilala, ikawa vile dhiaka.
Tukapiga yetu sala, likawakata choka.
Limekua ni swala, maadamu tulichoka.
Tabasamu la wengi, walevi kupigwa kumbo.

ALSO READ:  JOSEPHAT LAKA: NITOE GEREZANI

Walikesha vilabuni, na kuasi ya wakuu.
Kajiosha kwa sabuni, sheria yanukuu.
Walichoenzi miwani, hivi majuto mjukuu.
Tabasamu la wengi, walevi kupigwa kumbo

Zogo kwa familia, ja maziwa ya kuku.
Walizoea kuvamia, ugomvi kila siku.
Wake sasa washangilia, wala hawana shauku.
Tabasamu la wengi, walevi kupigwa kumbo

Barakoa walisusia, kajisifia ati mababi.
Wamebaki kulia, sasa walinde mabibi.
Imepitishwa sheria, polisi ndio mababi.
Tabasamu la wengi, walevi kupigwa kumbo

Anajuta shetani, kupungukiwa wafwasi.
Warudi kanisani, ulevi ndio kuasi.
Wazame basi tobani, waepuke hiyo risasi.
Tabasamu la wengi, walevi kupigwa kumbo.

Avatar
Josphat Laka
Josphat Laka is a third year student at EGERTON UNIVERSITY taking bachelor of PROCUREMENT AND SUPPLY CHAIN MANAGEMENT, a freelancer and a poet.
http://aowapress24.com

Leave a Reply

Your email address will not be published.