SHAIRI LA WIKI.

MALENGA JOSPHAT LAKA: “HATARI MASHINANI.”

Sikizeni kwa makini, imeanza safari.
Imetoka HATARI MASHINANI., korona ni dhahiri.
Vitavua sikioni, naonya kwa shairi.
Hatari mashinani, yakodolea macho.

Magari yaja ko bara, tahadhari sijute.
Sisitizo tena mara, safika isikupate.
Imevuka mto Mara, sijishike upwete.
Hatari mashinani, yakodolea macho.

Wamejaa kinanyanya, sisahau mababu.
Serikali kwisha onya, sijiweke taabu.
Kazi yangu keshafanya, nasubiri jawabu.
Hatari mashinani, yakodolea macho.

Jukumu ni letu sote, tuwalinde wazazi.
Kinga tupateni sote, tuambiane wazi.
Gonjwa hili tusipate, tuweke vizuizi.
Hatari mashinani, yakodolea macho.

Tusiwe wa mapuuza, tutoke vikundini.
Habari ndo nawajuza, niwe huru moyoni.
Firimbi sa napuliza, leteni yo maoni.
Hatari mashinani, yakodolea macho.

ALSO READ:  SAUTI YA HAKI: WACHENI DHULUMA POLISI.

Kwa Mola nampa dua, tulinde waja wake.
Habari hizi sikia, hazitambui wake.
Tumebaki vumilia, kuomba twimarike.
Hatari mashinani, yakodolea macho.

Magavana jengeni, hospitali tayari.
Maji nayo mtupeni, wala sio hiari.
Kura zetu tuliwapeni, ondoeni hatari.
Hatari mashinani, yakodolea macho.

Nimefika kikomoni, uzima natakia.
Nafungua zangu mboni, Mola nategemea.
Naingia mafichoni, nizidi kupekua.
Hatari mashinani, yakodolea macho.

Avatar
Josphat Laka
Josphat Laka is a third year student at EGERTON UNIVERSITY taking bachelor of PROCUREMENT AND SUPPLY CHAIN MANAGEMENT, a freelancer and a poet.
http://aowapress24.com

Leave a Reply

Your email address will not be published.