NEWS SPORTS

Mashabiki wa Liverpool washerehekea Ubingwa Baada ya miaka 30.

Liverpool wametwaa ubingwa wa Ligi kuu nchini Uingereza wakiwa sebuleni wanakula bisi tu wakiwatazama Chelsea wakiwastahilisha adhimisho la ubingwa huo uliosubiriwa kwa miaka 30… Ubingwa uliotaka kutiwa doa na Corona lakini ukiwa ni furaha ya dunia ya wanamichezo🙌

Furaha ya dunia ya soka!? Ndio, wanamichezo wanapenda ushindani na kusingekua na msisimko kama City angetwaa kwa mara ya 3 mfululizo kwenye ligi inayotajwa Kama ligi shindani zaidi duniani ikizingatiwa zaidi na namna klabu ya Liverpool ilivyokosa ubingwa huo msimu wa 2013/14 na 2018/19 kwa kutibuliwa dakika za mwisho.

Liverpool imetwaa ubingwa huu kwa namna ya pekee kabisa ikiwa imesaliwa na michezo 7 ya Ligi kitu ambacho hakikuwahi kutokea kabla na ni ishara ya moja kwa moja kwamba mbio zake za ubingwa zilikua ni mbio bora zaidi na klabu ilijiandaa kutafuta ilichokipata. Woow!! Wamestahili ubingwa kwani wamepoteza mchezo mmoja tu dhidi ya Watford mpaka sasa na ni timu iliyofanikiwa zaidi msimu huu duniani miongoni mwa ligi za ndani.

ALSO READ:  "Raila and Gideon Moi are my political mentors. Steve Mbogo.

Ndoto ya Jurgen Klopp!? Ndio, Ni ndoto ya Klopp ambaye wakati anaanza kuhudumu kama kocha wa Liverpool miaka mitano iliyopita aliikuta klabu ikiwa nafasi ya nane na ikiwa imetoka kuukosa ubingwa dakika za mwisho akichukua pahala pa Brendan Rodgers aliomba miaka minne alete makombe na amefanikiwa kuwapa klabu bingwa Ulaya na klabu bingwa ya dunia. Amewapa makombe.

Ubingwa wa Ulaya haukuwa kiu ya Liverpool kuliko ubingwa huu. Una maana kubwa kwenye roho ya Bil Shank na wahafidhina wa pale Anfield. Una maana kubwa kwa Kenny Darglish, Jamie n.k. Ni ndoto iliyotimia.

ALSO READ:  Six key factors to consider in settling for Cyber Cafe Business Today. 

Kongole Liverpool kwa hili na bila shaka Jurgen Klopp ataimbwa kama shujaa wa Liverpool 🙌 Miaka 30 Sasa huenda ikawa mazoea kama Klopp atasalia Anfield. Shaka yangu ni hii furaha inaweza kutoa maamuzi ya “kushtua” (tusiyoyatarajia) kwa Jurgen🤝
Wasalaam

Nazareth J Upete
Nazareth J Upete
Nazareth Upete is a young Tanzanian journalist who believes in collective development, transparency, fairness and dignity. He is specialized in Sports and News writing. An anchor, reporter, analyst and columnist.

Leave a Reply

Your email address will not be published.