NEWS SPORTS

FRAGA KAMA MCHEZAJI WA SIMBA KULIKO KAMA MBRAZIL NA KURA YA MODRIC.

Mnamo mwaka 2012 kiungo wa Real Madrid Luca Modric alipata asilimia 32.2 ya kura za usajili “wa hovyo zaidi” kwenye La liga akimpiku Alexander Song aliyesajiliwa na klabu ya Barcelona ikiwa Luca alikuwa na wastani wa kucheza dakika 38 tu mpaka mwezi Disemba kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.

Wakati aliporudi kujiunga na timu ya taifa ya Croatia aliulizwa na waandishi wa habari kuhusu kura hizo akasema “Sijisikii vibaya kwa hilo na sitaomba radhi kwani nipo Real Madrid kwenye klabu kubwa na ni ngumu kuendana na mazingira ya klabu kubwa kwa haraka”.

Kilichofuata ni hiki tulichokiona kiasi cha kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia mbele ya Lionel Messi na Ronaldo.Hapa kwetu alisajiliwa Gerson Fraga kwenye klabu ya Simba na kuwa usajili gumzo baada ya Simba kuficha jina lake kwa muda wakati wakiitumia saa Saba yao kama ilivyokuwa utaratibu wao.

ALSO READ:  DP William Ruto beats Raila and Kibwana in the latest poll.

Mbrazil!? Ooooh!! Ilikua lazima iwe stori kubwa kwa urejeo wa wabrazil kama Santos wa Coastal Union, Jaja na Andrey Coutinho waliokuwa Yanga na wakaonekana kushindwa kuendana na mpira wetu ingawa Coutinho alionesha kitu.

kimataifa wa Brazil anayekipiga kwenye klabu ya Simba Sc nchini Tanzania. /PICHA HISANI/

Fraga hajapata muda mwingi wa kucheza lakini amefunga mabao manne na assist 2 kwenye mashindano rasmi msimu huu na Mara zote anapopata nafasi amekuwa akionesha ubora wake. Kwa uchezaji wake wa “Sitaki lawama na fedheha” umemfanya kuwa kiungo wa pekee na suluhu ya ukabaji kwa Simba ambayo Sven amechelewa kuijua na Kama angeijua mapema huenda angeshatibu tatizo la ukabaji kitaaambo.

Bado Kuna baadhi ya watu hawajamwelewa Sana lakini naamini ni ngumu kumuelewa Fraga hasa ikiwa utamtazama kama Mbrazil kuliko Kama mchezaji wa Simba… Anakaba kwa wakati na anaachia mpira haraka kutafuta eneo lingine la kupewa mpira. Sio rahisi kumwelewa mbrazili mgumu.

ALSO READ:  Ayub Savula Reveals Details of How ODM Wanted him to Overthrow Musalia Mudavadi

Tunataka wabrazil wawe kina Gaucho na De Lima!! Fraga ni mchezaji Sana tu.

Naona bado Simba ina uhitaji wa kiungo huyu na natamani acheze na Mkude pale kati Kati ili kutengeneza utulivu kwenye kiungo Cha Simba.

Huenda hata hapa tungepiga kura kipindi kile “wabrazil” wangepigiwa kura za Modric. Tuhukumu kiwango chake na si uraia wake.
Wasalaam

Nazareth J Upete
Nazareth J Upete
Nazareth Upete is a young Tanzanian journalist who believes in collective development, transparency, fairness and dignity. He is specialized in Sports and News writing. An anchor, reporter, analyst and columnist.

Leave a Reply

Your email address will not be published.