POEM

TUMCHANGIE ASOME.

Mbiu hino ya mgambo, kwa sauti kuu yalia.
Bila shaka lipo jambo, ulonacho changia.
Tujitome kwenye chombo, mkonowe shikilia.
Tumchangie asome, MUTUKU LAZARO.

Nyota yake thiologia, atufanyie mahubiri.
Kwa moyo saidia, na mibaraka subiri.
Ata kama ni mia, itakuwa ni fahari.
Tumchangie asome, MUTUKU LAZARO.

Ni Mpole wa moyo, tena mwimgi wa furaha.
Tusiwe basi wachoyo, tujitokeze kwa madaha.
Tupige sasa zetu nyayo, isiwe ni karaha.
Tumchangie asome, MUTUKU LAZARO.

Wimbo wake ni wokovu, nazo sifa kwa Mola.
Kuondoa makovu, njia bora hasa sala.
Tumwombee kwa nguvu, tuseme Mola tawala.
Tumchangie asome, MUTUKU LAZARO.

ALSO READ:  SHAIRI : HARUSI SI WINGI

Siwi mwingi wa maneno, nifanyalo kusisitiza.
Tuungane yote mikono, bila shaka tunaweza.
Kuhimiza kwa maneno, ni sawa kumtuza.
Tumchangie asome, MUTUKU LAZARO.

Picha yake kaweka, msiseme hatumjui.
Biblia ameishika, wapi shangwe sisikii?
Kalamu imekatika, changeni nawasii.
Tumchangie asome, MUTUKU LAZARO.

Avatar
Josphat Laka
Josphat Laka is a third year student at EGERTON UNIVERSITY taking bachelor of PROCUREMENT AND SUPPLY CHAIN MANAGEMENT, a freelancer and a poet.
http://aowapress24.com

Leave a Reply

Your email address will not be published.