POEM

TWAKUPENDA MWALIMU

TWAKUPENDA MWALIMU.

Ni furaha moyoni, nikumbukapo nyakati.
Zile zama shuleni, mwalimu wetu wa dhati.
Aliboreka ata afisini, jinale Bwana MUTETI.
Twakupenda mwalimu, barikiwa daima.

Alidumisha nidhamu, upendo nayo amani.
Alipenda yake kalamu, milele nitamthamini.
Alifanya majukumu, vyema kutoka moyoni.
Twakupenda mwalimu, barikiwa daima.

Tabasamu aliweka, kila mara darasani.
La heri nazo fanaka, tutakuweka duani.
Uwe na mingi miaka, uhishipo hapa duniani.
Twakupenda mwalimu, barikiwa daima.

Alikuwa awali naibu, hivi sasa mwalimu mkuu.
Atatufanyikapo mababu, takuenzi kwa makuu.
Pendo lake la ajabu, ndio hivi nanukuu.
Twakupenda mwalimu, barikiwa daima.

ALSO READ:  SHAIRI : HARUSI SI WINGI

Bihashara jogirafia, anafunza kwa umahiri.
Mazuri twakutakia, kila mara nitakariri.
Na watu wote sikia, nimeandika shairi.
Twakupenda mwalimu, barikiwa daima.

Nitaishi kusimulia, utu wake wa kufana.
Kwa maneno asilia, nimsifu tena sana.
Hivi sasa namalizia, nitakumbuka ja jana.
Twakupenda mwalimu, barikiwa daima.

Avatar
Josphat Laka
Josphat Laka is a third year student at EGERTON UNIVERSITY taking bachelor of PROCUREMENT AND SUPPLY CHAIN MANAGEMENT, a freelancer and a poet.
http://aowapress24.com

Leave a Reply

Your email address will not be published.