UFICHUZI: Kwa nini Messi na Ronaldo sio Pele na Maradona.

GLOBAL NEWS SPORTS
Spread the love

Tupo katika dunia ya Ubishani. Dunia ipo katika mjadala wa je, ni Messi,Ronaldo,Maradona au Pelle ndio wachezaji bora kuwahi kutokea ulimwenguni!? Achana na Zinadine Zidane, Ronaldinho Gaucho, Michel Platin, Bebeto na Romario ama Ronaldo De Lima… Hawa nao wana daraja lao.

Nyota wa zamani wa Brazil mshambuliaji Ronaldo De Lima |PICHA HISANI|

Mjadala huu umekua ukigubikwa na Nyakati walizoishi waliowashuhudia nyota hao. Yote kwa yote Mimi naamini huenda Vipaji vyao havijatofautiana sana ila Nyakati, Sheria na Maendeleo ya mchezo wa Soka ndio yanaleta mitazamo hii.

Kuanzia miaka ya 2005 mpaka wakati huu mchezo wa soka umekumbwa na mabadiliko makubwa… Umekua ni mchezo unaotaka timu nzima icheze zaidi na sio vipaji binafsi. Nafasi ya vipaji binafsi inabaki kama njia mbadala ya utafutaji wa matokeo katika soka!!

Nyakati za “madenge na mpira madenge na mpira” zimeisha sasa ni soka la wote. Nipe nikupe imefanya tusione saaana uwezo halisi wa mchezaji husika.

ALSO READ:  Inside the 97 minutes of terror, Lampard tastes vinegary liquor at Wembley.

Lionel Messi na Cristiano Ronaldo naamini kuna vitu hawajatuonesha kutokana na mabadiliko ya Soka. Wakati Dunia ikistaajabu ya Lionel Messi kupasiana penati tayari Cruyff alishafanya. Ronaldo kupaa hewani tayari Francos Biyk Cameroon alisharuka mizania ile mwaka 1990 (pichani) kwenye kombe la dunia alipowafunga Argentina…

Mshambuliaji wa Cameroon Francos Byik akiruka mizani baada ya kufunga bao dhidi ya Argentina katika kombe la dunia 1990 |PICHA HISANI|

Tunaona ni vipya kwa sababu mifumo ya soka la sasa haimtaki Ronaldo atuonyeshe alichozaliwa nacho bali alichofundishwa zaidi. Mtazame Lionel Messi akikimbia na mpira. Anakufurahisha sana lakini hatafanya sana hata kama nafasi ipo ni kwa sababu dunia ya mpira inamtaka apasie mwingine na watu wote uwanjani waguse Mpira. Kucheza mwenyewe ni mpaka timu ishindwe kabisaaaaa.

Kama ingelikua mfumo wa soka unaendelea kuhitaji kipaji uwezo binafsi naona dhahiri Messi na Ronaldo wangeshatufanyia mambo ambayo tunasema walifanya kina pelle na maradona ama Kina Romario.

ALSO READ:  Three Aurora police officers fired for taking selfie photos next McClain memorial.

Soka la zamani lilikua na Ubabe. Ndio, lakini Pelle alikua na mwili mdogo tu. Watu wanacheza kulingana na mahitaji wa wakati huo. Itakua ni jambo gumu kuona mtu akitumia nguvu kubwa kwenye mchezo wa pasi nyingi.. Lazima naye aishi yaliyopo

Mahitaji na mifumo hii inazidi kuufanya mpira ule wa kina Romario na Bebeto kuwa tofauti na wa Neymar na Jesus. Wakati zamani Namba 9 akikaa juu kusubiri mipira sasa namba 9 anarudi kuokoa mipira langoni kwake. Ndio maana soka la sasa nambari Tisa wa kusimama wanahesabika kwa vidole.

Nyota wa soka duniani. Lionel Messi|PICHA HISANI|

Nafikiri tunapaswa kuheshimu uwepo wa Pelle na Maradona na wenzao ila tusiseme Messi na Ronaldo hawajawahi kuwafikia. Kila watu wametamba kwa Nyakati zao na Kwa mifumo yao na Kwa mpira wao.

Brenda HoloBrenda Holo
Brenda Holo

Brenda is obsessed with giving the audience something they don't see coming

Leave a Reply

Your email address will not be published.