GLOBAL NEWS SPORTS

Kutana naye Simon Msuva, Mtanzania mwenye roho ya Amerika ya Kusini.

Tazama hiyo picha ya Simon Msuva! Bila shaka inazungumza sana…. Inaweza ikulize ikiwa itapata matokeo tofauti na hisia hizo… Inaweza ikufurahishe kwa utayari na hisia ilizoweka kuelekea kwenye shughuli inayofuata… Ndio, huyu ndiye Simon Msuva aliyeng’aa ligi ya Tanzania bara kwa misimu 3+ kisha akaenda ng’ambo na bado anafanya vizuri kwa sasa akiitumikia klabu ya Hassan Difaa El Jadid ya Morocco ana kitu cha ziada anachokifanya.

Kikosi kizima cha timu ya Difaa El Jadido ya Morocco |PICHA HISANI|

Msuva ni miongoni mwa Watanzania wachache wasiokata tamaa… Amepitia nyakati nyingi ngumu mno. Mechi yake ya kwanza ya ‘Kariakoo derby’ hakuimaliza! Alilimwa kadi nyekundu. Ikaaminika ana mapenzi na upande wa pili…. Kuna nyakati alitoka uwanjani akitokwa na machozi. Nyakati ngumu kwake huenda zilikua ni wakati wa makutano ya watani wa jadi wa soka la Tanzania, Msuva hakukata tamaa.

Kiungo wa Kati, Mtanzania Simon Msuva akisherehekea baada ya kuguza nyavu ligini Morocco |PICHA HISANI|

Alijitolea kuipigania Yanga katika nyakati zote kama kawaida na hata pale jitihada za baadhi ya watu kumuhusisha na ushabiki wa Simba hakuwahi kujibu zaidi ya kupambana. Kuna mechi ya Yanga dhidi ya Simba alitolewa mapema sana ndani ya kipindi cha kwanza lakini hakuonesha kiburi zaidi ya kujiimarisha azidi kuwa bora… Msuva hakuwa kama Yikpe Gnamien ambaye Klabu ya Yanga ni kama inajuta kumsajili kutoka Gor Mahia alikovunja mkataba hapo awali.

ALSO READ:  U.S Records a Sharp Economic Downturn not Witnessed in Years

Mshambuliaji wa zamani wa Gor Mahia Yikpe Gnamien hajaonyesha ubabu wake kwenye klabu ya Yanga |PICHA HISANI|

Ni ukweli usiopingika mechi za watani wa jadi nchini Tanzania; Simba na Yanga zina presha kubwa lakini msuva aliimudu. Watu walimkosoa sana wakamuita si mchezaji mzuri, wengine walisema ataishia Yanga lakini aliwapuuza na kuganga yajayo.

Baada ya kukamilisha uhamisho wake kwenda Difaa El Jadid ndio kama watu waliwaza ni lini atarudi kujiunga na simba ama Yanga japo wachache walimpa nafasi ya kusonga mbele zaidi. Msuva aliwapuuza.

Hakupata namba mapema timu ya taifa. Hakukata tamaa napo alizidi kupambana. Kwa sasa ni miongoni mwa nyota wawili wa mfano nchini sanjari na swahiba wake Mbwana Samatta ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania – Taifa stars.

ALSO READ:  Three Aurora police officers fired for taking selfie photos next McClain memorial.

Mshambuliaji tajika wa Genk FC Mbwana Samatta ambaye pia ni nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars). Zipo taarifa zinazohusisha na uhamisho Brighton FC ya Uingereza |PICHA HISANI|

Simulizi yake inaumiza zaidi kuliko kufurahisha kwani watanzania wengi hushamirishwa na sifa ya kukata tamaa lakini Msuva amekuwa kama Mchezaji wa Afrika Magharibi ama Marekani ya Kusini wachezaji ambao hawakati tamaa kirahisi wakiamua kulipigania jambo.

Kila la kheri Msuva. Wenzio huku hawaoni kama kuna maisha mengine zaidi ya Simba na Yanga. Wameamua kuishia hapo.
Wasalaam.

Brenda Holo
Brenda Holo
Brenda is obsessed with giving the audience something they don't see coming

Leave a Reply

Your email address will not be published.