ABDALLAH SAID NA AKILI YA PLUIJM KATIKA FIKRA ZA MANJI NA WATANZANIA…. Dr

NEWS SPORTS
Spread the love

Usiku mmoja wa April 2016 nchini Misri katika Uwanja mkubwa wa Borg El Arab mjini Alexandria wenye masaa sawa na saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki klabu ya Yanga kutoka nchini Tanzania ilikua inakwaana na klabu ya soka ya Al Ahly mabingwa wa kihistoria wa michuano ya klabu bingwa barani Afrika katika mchezo wa mashindano hayo.

Ndio, mchezo wa mtoano ulioshika hatamu nchini Tanzania na Misri lakini Misri kulikua na Gumzo kubwa kutokana na matokeo ambayo klabu ya Yanga iliyapata mwaka mmoja kabla wakati iking’olewa na Al Ahly kwa mikwaju ya penati huku “Panenka” ya Nahodha wa klabu ya Yanga Nadir Haroub ikizungumzwa zaidi kuliko uwezo wa Deogratius Munish aliyeokoa penati na walizokosa Yanga.

Hofu ilikua nini!? Yanga ilikua inawakosa Mbuyu Twite, Salum Telela naye hakuwa na utimumu sahihi na Mwinyi Hajji ambao walishaanza kuiva kikosini hivyo Yanga wakalazimika kumtumia Kamusoko pekee kama kiungo mwenye uwezo mzuri wa kukaba alaf Oscar Joshua acheze upande wa kushoto na huku ndio kulionekana kungewapa nafasi Al Ahly kwa makosa aliyokuwa nayo Joshua kabla ya mchezo ule…

ALSO READ:  MASON GREENWOOD BETWEEN WAYNE ROONEY AND JACK WILSHERE.

Yanga wanaanza kwa kushambulia kwa nguvu mno na kuwatisha kina Ahmed Fathi na Rami Rabia waliokuwa wakicheza kama mabeki wa pembeni kwa kasi ya Simon Msuva na Deus Kaseke huku Haruna Niyonzima akikimbia kila upande ulipo mpira… Kiwango maridadi kabisa jamanii…. Wenyeji waliduwazwa kiasi na Thaban Kamusoko. Alicheza taratibu tu akikaba njia zao na kutoa pasi sahihi mno kwa wenzie.. Yanga walijikoki kweli kwelii.

Mnamo dakika ya 52 kichwa kikali cha nahodha wa Al Ahly Hossam Ghaly akiunganisha kona ya Ahmed Fathi kilikua ni kutaka kuwakatisha tamaa watanzania walioamini kwa kiwango cha yanga ile kule misri ingeweza kufanya chochote na kweli… Juma Abdul “anamchetua” Rami Rabia na kuweka krosi ndogo inayounganishwa kwa umaridadi na Donald Ngoma na kufufua natumaini ya watanzania…

Yanga wakiamini wanaongezewa dakika 30 zaidi ili kwenda kuamua hatma yao… Ni dakika ya 90+4′ Abdallah Said anaunganisha krosi safi ya “kipara” Walid Soliman… Ngoma inaishia jukwaani 2-1 yanga kapoteza!! Akili ya kocha Hans Pluijm wa Yanga ilimtesa mno Mwarabu siku hii… Alipambana mno… Alistahili ile kauli ya “tumekufa kiume”.

ALSO READ:  Tokyo Olympics: Lord Coe supports athletes right to take a knee

Haikuwa Simanzi ndogo ila ilimezwa na mshangao wa soka walilolionyesha vijana wa Yanga… Ilionekana kama Vilabu vyetu vinaweza kuwatikisa waarabu kwani Azam licha ya kutolewa na Esperance siku moja nyuma lakini pale Chamazi aliibuka na ushindi wa bao 2-1. Tangu hapo maisha yameenda kasi… Lile tumaini la Yusuf Manji kuiona Yanga ya Usiku ule lilipotea… Mashabiki wa mpira hawajui ni lini wataiona Yanga ile ya pale Alexandria… Watanzania walau walifutwa machozi na Simba ila Kwa ile Yanga ilitarajiwa kufanya jambo… Haijawa hivyo. Itakua hivyo lini!? Muda ni Hakimu mzuri.
Gracias

Brenda HoloBrenda Holo
Brenda Holo

Brenda is obsessed with giving the audience something they don't see coming

Leave a Reply

Your email address will not be published.