‘OKWI’ NA NIYONZIMA NA DHANA YA ‘UPRO’

SPORTS
Spread the love

Utamwambia shabiki gani wa soka la Afrika Mashariki kuhusu Ubora wa Haruna Niyonzima akubishie!? Nani anaweza kusimama hadharani akatuambia Emmanuel OKWI ni mchezaji wa kawaida tu!? Bila shaka hapana.

Si tumekubaliana hilo!? OK. Tuendelee… Okwi aliingia nchini Tanzania mnamo mwaka 2009 wakati Haruna aliingia mwaka 2011 ikiwa ni moja tu ya kazi ya Abdallah Bin Kleb aliyekuwa akimfuatilia Haruna akiwa na kikosi cha APR akionekana ni kijana mwenye kila aina ya kipaji na umaridadi.

Okwi yeye alionwa pale Uganda na ilikua ni kipaji kikubwa akicheza upande wa kushoto wa klabu yake naye alikua angali Yu mvulana. Hawa wawili kwangu ndio wachezaji bora zaidi wa Kigeni kupata kuwaona ingawa kiasi ntamfikiria Kipre Herman Tcheche aliyekuwa kwenye klabu ya Azam Fc.

Haruna na Okwi wanafanana sana tu mpaka usumbufu kwa mabosi wao. Wakienda kujiunga na timu zao za taifa kurudi kwa wakati huwa ni suala gumu sana. Kinachokuja kuwadogolesha mabosi ni hawa jamaa wakiwa uwanjani. Haruna atapiga pasi kaskazini na macho yake yalitazama jua la magharibi na Okwi atafunga akiwa ameshakoswa na miguu ya walinzi wanne. Hawachoshi kukuudhi kwa wiki moja na kukufurahisha mwezi mzima🤣!

ALSO READ:  Chris Smalling: Man Utd defender joins Roma on a permanent deal

Alaf hawa jamaa kwenye maslahi wao hudai kweli kweli… Huwa wanavumilia njaa kwa ‘machale’ na mahesabu yao. Niyonzima akisaini sehemu ujue kashanusa dalili ya hela. Okwi anaposaini sehemu jua kashachungulia kesho. Si unakumbuka Niyonzima alivyowatosa wanajangwani na Okwi aliwatosa waarabu wenye visima vyao vya “wese la petroli!?”

Ni ngumu kumuuliza Niyonzima utamaduni wa Rwanda akakupatia jibu kama atakalokupatia Olivier Kalekezi. Hata Okwi ukimuuliza utamaduni wa Uganda hatakujibu kama utakavyojibiwa na Tonny Mawejje. Wao wamekulia Tanzania, Wanaishi Tanzania na wanapendwa Tanzania.🙌

Si nilikuambia usumbufu wao!? Hawa jamaa ukitaka kuwatema usiwape mechi ya ‘tuone’, watakuumbua wateme jumla. Wakati Yanga wakimpiga kuti kavu Haruna alipoomba msamaha walimrudisha dhidi ya Prison akiingia dakika ya 66 lakini alipiga pasi 28 zaidi ya mchezaji yoyote aliyeanza na kutoa assist 1. Kwa Okwi alipewa mtego kama huo dhidi ya Singida United jioni kwa mkapa… Aliwageuza Singida ng’ombe wa shughuli akitupia mbili na Singida ilikua ile yenyeweee… Ya Danny Usengimana, Rusheshangoga, Batambuze n.k

ALSO READ:  ASENSIO KATIKATI YA GALACTICO NA MWISHO WA HADITHI YA MADRID.

Tunakubaliana kuwa hawa jamaa kama binadamu wengine hawajatimia. Wana mapungufu yao lakini isitupatie uzito kusema hawa ndio waliofanikiwa kuwakonga nyoyo watanzania kwa miaka kumi na kujijengea umaarufu kila upande.

Tunavyotafuta wachezaji wa kulipwa ‘mapro’ ni vyema tungepata Okwi na Niyonzima wengi hasa wa Uwanjani wanaoweza kudumu katika ubora wao kwa miaka 10 au zaidi ili tulete dhana halisi ya Ushindani na wazawa wajifunze. Hawa kina Yikpe na kina Wilker aaaa hapana….

Hawa “tumepigwa”.
Wasalaam
Instagram: @nazareth.j.upete

Brenda HoloBrenda Holo
Brenda Holo

Brenda is obsessed with giving the audience something they don't see coming

1 thought on “‘OKWI’ NA NIYONZIMA NA DHANA YA ‘UPRO’

Leave a Reply

Your email address will not be published.