๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Kipindi kinaganaga,nanga sasa kimeng’owa
Mtama leo kumwaga,tumwage bila shakawa
Mambo kinagaubaga,yote kuyaweka sawa
Mgeni wetu waziri,karibu mheshimiwa.
Kwanza kunazo tetesi,wizi wa kura kuhusu
La pili kunazo kesi ,wapinzani maabusu
Wana nti limewaghasi,uimla kupa busu
Kuongoza umefeli,wanasema wapinzani.
๐๐๐๐๐๐๐๐
Ninashukuru kijana, kunipa hii nafasi,
Niwaeleze bayana, walizozua tetesi,
Hivyo basi kwa upana, nitasema bila wasi,
Asante mwanahabari, kunipa huu wasaa.
Upinzani hao waongo, wasemayo si ukweli,
Wameishiwa mipango, mbinu zao zimefeli,
Wanapakaza uongo, watutoe kwenye reli,
Siasa hawaiwezi, kura wanaibiwaje.
Ni wazi hawana hoja,uzalendo na nidhamu,
Kazi kufanya vihoja, katika zao awamu,
Kazi yao ngoja ngoja, washazichoka kaumu,
Hao hawanazo sera, kazi yao kulalama.
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Wanalia wapinzani,haki zao wamenyimwa
Wengi wamo gerezani,watetezi wamezimwa
Bila sauti kinzani,Mtatufanya watumwa
Upinzani wauliwa,wanasema wadadisi.
๐๐๐๐๐๐๐๐
Maneno ya wadadisi, hayo hayana mashiko,
Yamekosa ufanisi, hayaleti muamko,
Hivyo kwa jibu rahisi, yatatupeleka siko,
Sisi bila ubaguzi, tunatoa haki sawa.
Jua hata awe nani, atapovunja sheria,
Huwa anawekwa ndani, akutwapo na hatia,
Liwe funzo asilani, kosa kutolirudia,
Hivyo awe mpinzani, ama wa chama tawala.
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Kamera haimuliki,kuonesha hali kweli
Sauti haisikiki,kiwaulizeni swali
Kalamu haiandiki,kuanika matapeli
U wapi Uhuru wetu,Waandishi wa habari?
๐๐๐๐๐๐๐๐
Kukosoa pasi kosa,kila tunalolitenda
Ya pesa nane siasa ,iwateni propaganda
Tutawadhibiti sasa,ndo mkome kutuponda
Kaburini la sahau,uhuru wa pinga pinga
๐๐๐๐๐๐๐
Usemayo mvunda nti,zako hoja twasikia
Hutoweza tudhibiti,wala kuvunja sheria
Tena kura haupati,debeni utajutia
Uhuru mlofukia,lazima tutafufua.
๐๐๐ญ๐ฎ๐ง๐ณ๐ข;
๐๐๐๐ฎ๐ฆ๐ ๐ค๐ก๐๐ฆ๐ข๐ฌ
๐๐ฌ๐ก๐๐ข๐ซ๐ข ๐ฆ๐๐๐ก๐ข๐ง๐ ๐
๐๐๐ซ ๐๐ฌ ๐ฌ๐๐ฅ๐๐๐ฆ ,๐๐๐ง๐ณ๐๐ง๐ข๐
๐
๐๐ฅ๐ข๐ฑ ๐. ๐๐๐ญ๐ฎ๐ฆ๐จ
๐๐๐ฅ๐๐ง๐ ๐ ๐ฆ๐ญ๐๐ฆ๐ฎ
๐๐๐ซ๐ฎ,๐ค๐๐ง๐ฒ๐.